2 Julai 2025 - 13:29
Source: Parstoday
Waislamu na wafuasi wa Palestina wanakandamizwa katika vyuo vikuu vya Canada

Waislamu na waungaji mkono wa Palestina wanakabiliwa na vitendo vya ukandamizaji katika vyuo vikuu vya Canada.

Ripoti zinaonyesha kuwa, Canada, kama zilivyo nchi zingine za Magharibi, nayo imekuwa ikikandamiza sauti za wafuasi wa Palestina baada ya kuunga mkono bila masharti jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sambamba na sera ya kuwakandamiza Waislamu na wafuasi wa Palestina, Wizara ya Elimu katika mkoa wa Quebec unaozungumza Kifaransa imechapisha ripoti inayodai kuwa, kumbi za sala katika vyuo vikuu zinachochea mgawanyiko kati ya wanafunzi.

Ripoti hiyo ambayo iliwalenga zaidi wafuasi wa Palestina katika vyuo vikuu viwili vya umma mjini Montreal, ilidai kuwa, uuzaji wa nguo za Wapalestina katika chuo kikuu hicho, pamoja na kozi za lugha zinazohusiana na utamaduni wa Wapalestina, vinasababisha mifarakano kati ya wanafunzi na walimu.

Mamia ya raia nchini Canada wamekuwa wakiandamana mara kwa mara katika mji mkuu Ottawa na miji mingine ya nchi hiyo ya bara Ulaya na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kulaani mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza.

Madola ya Magharibi licha ya kutoa nara za usawa na haki za binadamu, lakini yamekuwa yakiongoza katika kukandamiza na kukiuka haki za binadamu kiasi kwamba, jamii za waliowachache au hata wafuasi wa dini za waliowachache hazina uhuru kabisa katika mataifa hayo. Jamii za waliowachache katika mataifa hayo zimekuwa zikibinywa na kukandamizwa kwa kila namna na hazina uhuru kabisa hata wa kuchagua aina ya nguo ya kuvaa, kutekeleza ibada zao na shughuli zao za kidini.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha